Wanasiasa katika Kaunti ya Mombasa hawaturuhusiwa kupiga kampeni na kuzungumza mambo ya kisiasa wakiwa katika majengo ya ibada.
Kauli hii imetolewa kwa mara nyingine na Askofu wa Kanisa la Kianglikana dayosisi ya Mombasa Julius Kalu.
Akizungumza siku ya Jumapili, Kalu alisisitiza kuwa jambo hilo litasaidia pakubwa kuweka nyumba za ibada kando na maswala ya kisiasa nchini.
“Wanasiasa wanapaswa kuheshimu nyumba za ibada na kukoma kurushiana maneno na kukemeana kisiasa wakiwa katika maombi,” alisema Kalu.
Wakati huo huo, amewataka wananchi kuwa huru kuchagua viongozi wanaowataka, pasi kushurutishwa.