Naibu kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Christopher Wanjau, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kutumia mbinu mwafaka kufanya kampeni zao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumanne, kamishna huyo aliwahimiza wanasiasa hao waache kutotumia mbinu za uchochezi kujinyakulia uungwaji mkono. 

"Hatutaki kupatwa na visa kama vya mwaka wa 2007/2008, wanasiasa msambaze amani," alisema Wanjau. 

Aidha aliwataka viongozi hao wawe mfano mwema kwa viongozi wanaoibuka kwa kufanya maendeleo badala ya kuleta chuki na ukabila.

"Viongozi wema ni wale wanaongoza kwa mfano mwema, wasemayo na watendayo," alisema wanjau. 

Wanjau aliwaomba wananchi kutowaunga wanasiasa ambao wanataka kuwagawanyisha kwa msingi ya kikabila. 

"Hatutakubali viongozi wenye nia ya kugawanya Kenya na kuleta machafuzi," alisema Wanjau.