Wanasiasa wazembe wanafaa kutemwa nje katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu ujao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na mwanasiasa Johnson Mwamba, ni jambo la kusikitisha kwa wananchi kuteseka miaka mitano baada ya uchaguzi. 

Akizungumza Jumatatu na wanahabari mjini Nakuru, Mwamba alisema kuwa wakati ni sasa kwa wananchi kuwapiga msasa viongozi. 

Hata hivyo, ametoa wito kwa wakaazi wa kaunti ya Nakuru kuepuka siasa za ukabila na kununuliwa kwa fedha.

"Siasa za ukabila na pesa zilishapitwa na wakati, watu wazembe hawafai kuchaguliwa uchaguzi mkuu ujao, viongozi wachunguzwe vizuri kabla ya kupigiwa kura," alisema Mwamba. 

Wakati huo huo, ametoa wito Kwa viongozi waliopo mamlakani wawajibike zaidi na kuhakikisha wanatimiza wanaowawakililshi ahadi walizowapa.

Picha: Mwanasiasa Johnson Mwamba. Amewataka wananchi kumakinika na kuwafanyia wakazi kazi.