Ilikuwa ni shangwe na nderemo wikendi iliyopita katika kituo cha kujigua akina mama cha Bondeni Nakuru wakati walipotembelewa na muungano wa wanaume wakatoliki CMA.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongozwa na Enrique Nyangonga, wanachama hao wa CMA Nakuru walikuwa na ujumbe Kwa akina mama hao.

"Lengo letu kuu la kuzuru hapa ni kuhakikisha kwamba familia ina nguvu na umoja," Nyangonga alisema.

Wakati wa ziara hiyo akina mama waliojifungua katika kituo hicho walipokezwa bidhaa mbalimbali za matumizi.

"Kwa niaba ya akina mama hawa na kituo hiki ningependa kushukuru sana muungano wa wanaume wakatoliki CMA Kwa kuzuru kituo hiki na kuonyesha upendo, " Salome Gachathi alisema.