Wanaume wawili wamefikishwa katika mahakama ya Ogembo kaunti ya Kisii kwa kuweka picha za naibu gavana wa kaunti Joash Maangi akiwa uchi wa mnyama katika mtandao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanaume hao Samson Ogendi na Joseph Nyang’au wanadaiwa kuweka picha hizo mtandaoni tarehe 8 mwezi huu.

Washukiwa hao hawakusomewa mashtaka yao baada ya kusema maafisa wa polisi waliwanyima haki zao kwa kuwanyanganya pesa walizokuwa nazo, simu pamoja na nguo.

Jaji wa mahakanma hiyo W.K. Chebsuba aliagiza washukiwa hao kuwekwa korokoroni ili uchunguzi kufanywa kabla ya kusomwa kwa mashtaka yao.