Wanawake katika eneo la Changamwe wamelalamikia ongezeko la visa vya ubakaji na ulawiti katika eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na mwanasiasa kutoka Mombasa Safiya Dima, wanawake hao walisema kwamba mitaa ya Magongo, Chaani, Migadini, na yale ya Wayani katika eneo hilo yamekuwa yakishuhudia visa vya watoto wadogo kudhulumiwa kingono.

Akizungumza katika eneo la Changamwe, Bi Dima alisema kuwa hali hiyo inasikitisha mno huku akiongeza kuwa ni lazima idara husika ziwajibikie tatizo hilo vilivyo ili kuwalinda watoto wadogo dhidi ya uovu huo.

“Tunaishi kwa hofu. Kama kina mama tunapaswa kulindwa na idara husika lazima ziamke na kulishughulikia swala hili mara moja,” alisema Bi Dima.

Dima hata hivyo aliwakosoa baadhi ya wazazi wasiotekeleza majukumu yao ya ya kuwalinda watoto kikamilifu, huku akiwataka kuwa waangalifu zaidi hasa wakati huu wa likizo ndefu.