Wanawake wawili wenye umri wa makamo walifikishwa mbele ya mahakama ya manispaa ya Eldoret siku ya jumatatu na kushtakiwa kwa kosa la kuuza pombe haramu.
Julia Too na Witney Jepkoech walishtakiwa kwa kosa la kutengeneza pombe haramu katika eneo la Langas.
Washukiwa hao,walikamatwa na pombe haramu na afisa mkuu Anthony Alwanyi pamoja na askari wa Kaunti ya Uasin Gishu siku ya juma pili.
Mahakama ilielezewa kwamba,wawili hao walinaswa baada ya wananchi kuwaambia askari wa kaunti.
Aidha, wawili hao walikubali mashtaka hayo na kumuomba hakimu mkuu mkaazi mheshimiwa Pauline Mbulika kuwaachilia kwa dhamana kwani walikuwa na watoto wadogo nyumbani.
Julia alipigwa faini ya Sh.40, 000 ilhali Witney alipigwa faini ya Sh. 50,000.
Emily Jelagat ,mwenye umri wa makamo alifikishwa mbele ya mahakama hiyo siku ya ijumaa baada ya kunaswa na lita 200 za Kangara katika eneo la Jasho farm katika kaunti ya Uasin gishu.
Hakimu mkuu mkaazi mheshimiwa Pauline Mbulika alimuamuru Emily kulipa dhamana ya Sh.200,000 au kifungo cha miaka mitatu gerezani.