Share news tips with us here at Hivisasa

Wanawake katika Kaunti ya Mombasa wamehimizwa kuzingatia muda uliyosalia wa kujisali kama wapiga kura ili kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.

Mbunge mteule katika Bunge la Kaunti ya Mombasa Caroline Owino, alisema kuwa takwimu inaonyesha kuwa idadi iliyojitokeza kusajiliwa kama wapiga kura ni ndogo mno ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Mbunge huyo alisema kuwa wanawake wengi bado hawajajitokeza kusajiliwa.

Akizungumza mjini Mombasa katika Kongamano la wanawake siku ya Jumatano, Ouma alisema kuwa wakati umefika kwa akina mama kuchukua fursa ya kujisajili ili kuwachagua viongozi wanaojali maslahi ya wanawake na kuwawezesha kufanikisha malengo yao.

"Takwimu inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wanawake bado hawajajitokeza kujisajili kama wapiga kura na nyinyi ndio mnaweza kuwachagua viongozi wanaojali maslahi ya wanawake, na kubadilisha uongozi duni Mombasa. Nawaomba mjitokeze na kujisajili kama wapiga kura,” alisema Ouma.

Shinikizo la Bi Ouma liliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya bunge la Mombasa kuhusu Vijana, Michezo na jinsia Bi Sarah Nyamvullah.