Afisa wa shirika la Haki Africa Salma Hemed akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Picha/ nation.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Imebainika kuwa idadi kubwa ya wanawake hawakushiriki zoezi la marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 katika Kaunti ya Mombasa kutokana na hofu ya kutokuweko na usalama wa kutosha.Kulingana na mshirikishi wa shirika la Haki Africa Salma Hemed, hofu hiyo ilitokana na jinsi siasa za marudio hayo ya uchaguzi zilivyoendeshwa na kuchangia kushuhudiwa kwa mgawanyiko nchini.Akiwahutubia wanahabari, Hemed alisema kuwa wanawake wengi walihofia kuwa huenda kukazuka fujo wakati wa chaguzi huo, hatua iliyochangia wao kutoshiriki katika zoezi hilo.“Wanawake waliogopa kushambuliwa na waliohofia usalama wao ndiposa hawakujitokeza kwa wingi,” alisema Hemed.Hemed alisema kuwa licha ya zoezi hilo kufanyika kwa njia ya amani katika Kaunti ya Mombasa, idadi kubwa ya wanaume pia ilikosa kujitokeza kupiga kura.Afisa huyo wa Haki Afrika amewasihi wanawake kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa mwaka 2022, ili kuleta mageuzi ikizingatiwa wanawake wengi wamekuwa wakitumiwa kwa maslahi ya kisiasa na viongozi wa kiume.Idadi ya wanaume waliojiandikisha kama wapiga kura Kaunti ya Mombasa ilikua asilimia 52.7 huku idadi ya wanawake ikiwa asilimia 47.3.Hata hivyo, katika uchaguzi wa Agosti 8, wanawake walijitokeza kwa wingi ikilinganishwa na idadi ya wanaume.