Hali ya sitofahamu imeibuka katika kivuko cha Likoni, baada ya wanawake kupendekeza kutengwe sehemu yao mwafaka wanapoiabiri feri. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Tetesi kuu ni kwamba kumeshuhudiwa visa vya dhuluma za kimapenzi kutoka kwa wapevushi ambao hutumia muda wa msukumano kama nyakati za asubuhi na jioni kutekeleza maovu hayo. 

Inadaiwa wanaume hawa hutumia muda wao kuvuka ng'ambo zote wakati wote wakiwadhulumu wanawake ambao wengi wao huyanyamazia matendo hayo.

Wanawake wamedai feri igawanywe sehemu tatu, moja yao, nyingine ya watoto na ya wanaume ili kupiga mkuki utovu wa maadili kama huu. 

Afisa mkuu mshirikishi wa mawasiliano Elizabeth Wachira alikubaliana na tetesi hizi.

"Tutakapopata feri mpya ambazo zimo njiani zitaingia wakati wowote, tutaamrisha kuwe na ya wanawake na watoto waabiri feri yao," asema Bi Wachira.

Pia alisema usimamizi wa kivuko hicho hauungi mkono kamwe visa kama hizi na mara kwa mara, kupitia vipasa sauti zao, huwaonya wenye hizi tabia potovu.