Hatua ya kutopitishwa kwa mswaada wa Thuluthi mbili na wabunge wa bunge la kitaifa umeibua hisia mbalimbali miongoni mwa viongozi wa kaunti  ya Mombasa hususan wanawake mashinani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Wanawake katika kaunti ya Mombasa Afiya Rama ameiitaja hatua hiyo kama inayolenga kudhalilisha uongozi wa wanawake na inaonyesha wazi kwamba wabunge hawatilii maanani uongozi wa wanawake hapa nchini .

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Afiya ameongeza kuwa ipo haja ya kuheshimiwa kwa uongozi wa mwanamke katika karne hii kwani wanawake wana uwezo wa kuongoza kama wanaume.

"Tunawaoma wabunge wa kiume kuunga mkono mswada wa usawa wa jinsia wa thuluthi mbili ili kuna kuwa swala ya usawa wa uongozi unatekelezwa vyema na kufanikisha maendeleo mashinani," alisema Afiya.

Kiongozi huyo wa wanawake amewaomba wabunge kuupitisha mswaada huo wakati bunge likaporejelea vikao vyake juma lijalo kama ilivyoratibiwa na spika wa Bunge la Kitaifa Justine Muturi.