Wanawake katika kanda ya Pwani wametajwa kuzubaa katika shughuli nzima ya kutafuta nyadhifa za uongozi nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wametajwa wengi kuwa hawataki kujihusisha na miradi ya kuleta maendeleo nchini kwa kile wanachokitaja kuwa wametelekezwa kwenye jamii.

Amina Rasul ni mwanaharakati na mkereketwa wa kisiasa katiaka eneo hilo na amesema kuwa wakati ni sasa wa kuamka kwa Wapwani kujikaza na kuingia kwenye ulingo wa kisiasa kutafuta nyadhifa mbalimbali.

Bi Rasul ameongeza kuwa wanawake ambao wako na elimu ya kutosha eneo la Pwani ni wengi ila wanaojihusisha na kutetea na kutafauta nyadhifa za uongozi ni kidogo ikilinganishwa na sehemu zingine kutoka bara.

Aidha ameongeza kuwa serekali za kaunti zikuja lakini idadi ya akina mama ambao hutafuta nafasi za kazi katika serekali hiyo pia ni haba.jamno ambalo limemkera kwa mda mrefu na ndio sasa amejitokeza kimasomaso ili kiliweka bayana jambo hilo wanawake wenzake waanze kuamka.

“Karne ya 21 lakini bado wanawake hatujamka bado,? ni jambo la aibu sana. Wamama na wadada tuamke kwa ukweli hii hali ni ya kutamausha, sauti ya Pwani sio wanaume pekee pia sisis tuko,” amesema Bi Rasul.

Hata hivyo tunastahili kushirikiana na serekali ya kaunti na mashirika mbalimbali ya kijamii kuhakisha kuwa ushauri nasaha umetolewa kwa kina mama na dada zangu.