Vijana na akina mama wameombwa kutohadaiwa na kufuata maadili ya kigeni ambayo huenda yakawapotosha kimaisha.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye mkao na wanahabari mjini Mombasa, Katibu mtendaji wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kiislamu nchini  (CIPK) Sheikh Mohammed Khalifa alisema kwamba mara nyingi vijana na akina mama hushawishika na kujihusisha na maadili yasiyostahili na kusababisha wengi wao kupitia halingumu ya kimaisha.

Sheikh Khalifa aidha aliongezea kuwa kuna haja ya jamii Pwani kujihusisha na maswala ya maadili mema bila kujali umri wao ili kupunguza visa vya utovu wa nidhamu.

Hata hivyo alisema kwamba kama viongozi wa kidini, hawataruhusu kuona wakaazi wa Pwani wanapotoshwa kimaadili.