Huenda visa vya kina mama wajawazito kufariki kabla na hata wakati wa kujifungua kwenye kaunti ya Mombasa, vikapungua licha ya kaunti hiyo kuorodheshwa kuwa kaunti inayoongoza katika visa vya kufariki kwa kina mama wajawazito kabla,baada na hata wakati wa kujifungua mkoani Pwani.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hii ni baada ya idara ya afya na matibabu kwenye kaunti hiyo kuanzisha mradi wa ujenzi wa vituo vya kushughulikia kina mama wajawazito kabla ya kujifungua (maternal shelter) naa kuboresha sehemu ya kujifungua katika hospitali eneo la Pwani.

Waziri wa afya kaunti ya Mombasa Abdi Mohammed amesema kuwa vifaa hivyo vitahakikisha kuwa maisha haipotezwi tena na kina mama wakati wa kujifungua.

Waziri huyo pia amewahimiza kina mama hasa kutoka mashinani mwa kaunti za Lamu, Kilifi na Kwale kutilia maanani umuhimu wa kujifungua kwenye vituo vya afya ili kuzuia vifo na hata matitizo kutokea.