Akina mama katika kaunti za Nyamira na Kisii wameshauriwa kuwa katika mstari wa mbele kubadilisha uchumi wa taifa kupitia biashara.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira Alice Chae, aliyezungumza mjini Nyamira siku ya Jumatatu,  alisema biashara ndio hubadilisha uchumi na maisha ya wengi katika taifa la Kenya, huku akiomba akina mama kujaribu kila wawezalo kuhakikisha maisha yao yameimarika zaidi kupitia biashara.

“Naomba akina mama kuenda kwa hazina mbalimbali za serikali na kupata mikopo na kufanya biashara ili kujiimarisha kimaisha na kubadilisha uchumi wa taifa,” aliomba Chae.

Wakati huo huo, Chae aliwaomba pia wanapopata mikopo hiyo kuitumia vizuri ili kutopata hasara, huku akisema huwa vyema wakati mkopo hutengeneza faida na kurudisha zile za mikopo kwa hazina zile wanazotoa pesa hizo.

“Mnapopata mikopo mhakikishe mikopo hiyo imebadilisha maisha yenu na sio kupata hasara wengi wamejiendeleza kupitia mikopo,” aliongeza Chae.