Akina mama katika kaunti ya Kisii wemeshauriwa kujitokeza na kuwania viti mbalimbali vya uongozi.
Kulingana na mwanasiasa kutoka eneo bunge la Nyaribari Chache Rachael Otundo, wanawake wana fursa ya kuwa viongozi hivyo basi amewashauri kutoogopa ila kuwania viti vya uongozi na kuleta maendeleo.
“Naomba akina mama ifikapo mwaka ujao mjitokeze katika siasa na kuwania viti ili kuchaguliwa kama vile wananaume huchaguliwa," alisema Otundo.
“Sisi akina mama tuna uwezo wa kuongoza, mimi mwenyewe ni mama ambaye nawania kiti cha ubunge Nyaribari Chache naomba wengine katika maeneo bunge yote tisa Kisii kujitokeza kuwania viti mbalimbali,” alisema Otundo.
Aidha, Otundo alisema si vyema wanawake kusubiri kuwania kile kiti Uakilishi Wanawake katika kaunti na kusema kila kiti kipo wazi na wana nafasi nzuri yakukinyakua.
Otundo aliomba viongozi wote wa kaunti ya Kisii kufanya kazi wakiwa pamoja ili kuhakikishia wakaazi wa kaunti hiyo wnapata maendeleo.