Huku Wakenya wakielekea katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, viongozi mbalimbali wamejitokeza na kuwashauri wanawake kujitokeza kwa wingi na kujitosa kwenye ulingo wa kisiasa ili kuchaguliwa na kuwafanyia wanawake wenzao maendeleo hadi mashinani.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Mombasa Mishi Mboko amesema kuwa wakati umefika sasa kwa wanawake kujitokeza na kujiunga na siasa ili kuchaguliwa na kuwafanyia wanawake maendeleo kwani katiba ya nchi inampa mamlaka kila mwanamke kufutaia demokrasia ya nchi huku akiwahimiza wanawake kujitokeza na kumchagua kiongozi mwenye kujali maslahi ya wananchi mashinani ili kuona kwamba maswala ya maendeleo mashinani yanaangaziwa vyema.

Akizungumza na wanawake kwenye mkutano wa wanawake wa maendeleo eneo la Likoni mjini Mombasa siku ya Ijumaa Mishi amewarai wanawake katika eneo hilo kuonyesha uiano na umoja na kuwachagua wanawake wenzao huku akisema kuwa wanawake ndio wenye kujali maslahi ya wakaazi wote hadi mashinani.

Mishi  amesema kuwa iwapo wanawake wote watajitokeza na kumchagua kiongozi moja mwanamke watakayempendekeza basi watakuwa wameonyesha uzalendo pamoja na kuheshimu viongozi wanawake kuwa wanaouwezo wa kubadilisha maisha ya Wakenya mashinani.

“Tafadhali akina mama msikukubali kudanganywa na baadhi ya viongozi wasiojali maslahi yenu jitokezene kwa wingi na muungane mchague kiongozi mwanamke mwenzenu ndio atawafanyia nyinyi mambo muhimu huku mashinani na kufanikisha maendeleo ya wanawake mashinani," alisema Mishi.