Wanaume wanne wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shatka la wizi.
Washukiwa hao, Judah Langat, David Kitonga, Welson Ngugi na Nicolus Bungua wanadaiwa kuiba kasha lililokuwa na mali yenye thamani ya shilingi milioni saba, mali ya Robert Muhira.
Washukiwa hao wanadaiwa kutekeleza wizi huo katika eneo la APM Terminal, katika eneo la Changamwe, kati ya tarehe 8 na 27, Mwezi Machi.
Wanne hao walikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Susan Shitub siku ya Alhamisi.
Hakimu Shitub aliagiza wanne hao kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano au shilingi milioni mbili pesa taslimu kila mmoja.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe Mei 30, 2016.