Share news tips with us here at Hivisasa

Wanaume wanne walifikishwa mbele ya mahakama moja ya Nakuru siku ya Jumatano kwa shtaka la jaribio la mauaji.

Wanne hao Dennis Nyakundi, Joseph Konesmas, Micheal Wanderi Na Isaac Kibe waliofikishwa mbele ya Hakimu Liz Gicheha wanadaiwa walijaribu kumuuwa Zachariah Mbui mnamo tarehe Octoba 5, 2015 kwa kumpa kichapo na pia kummwagilia petroli katika eneo la Kiratina viungani mwa mji wa Nakuru.

Hata hivyo, wanne hao walikanusha mashtaka haya huku wakitaka kuachiliwa kwa thamana na mahakama hiyo, wakijitetea kuwa wana familia zinazowahitaji.

Washtakiwa hao waliachiliwa kwa bondi ya Sh400,000 kila mmoja na mthamini wa kiwango sawia na hicho au Sh100,000 pesa taslimu kila mmoja.

Kesi dhidi ya wanne hao itatajwa tarehe Octoba 22, 2015 na kusikizwa tarehe Novemba 12, 2015.