Waziri wa ardhi kaunti ya Kisii, Moses Onderi, ameapa kupambana na wanyakuzi wa ardhi katika kaunti hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari, siku ya Alhamisi, baada ya kuzulu eneo la nyumba iliyoporomoka aliwaonya wezi wa mashamba ya umma wawe tayari kwa makabiliano na wizara yake.
“Serikali yetu itafanya kila juhudi kuona kuwa mashamba ambayo yamenyakuliwa kwa njia haramu yamerundishwa,” akasema Onderi.
Matamshi yake yalipigwa jeki na gavana, James Ongwae, ambaye alikuwa pamoja naye huku akisisitiza kuwa serikali yake haitalegea katika vita dhidi ya wanyakuzi wa ardhi.
“Kuwa tayari kukumbana na mkono wa sheria iwapo wewe ni mnyakuzi wa ardhi ya umma,” akasema Ongwae.
Ongwae pia aliwataka wakaazi kushirikiana na serikali yake kuinua maendeleo katika eneo hilo.
Msikubali kutumiwa na wana siasa kuharibu au kusimamisha maendeleo,” alisema Ongwae huku akirejelea maandamano yaliyofanyika mjini Kisii wiki hii.