Waziri wa ardhi katika Kaunti ya Kisii Moses Onderi, amesema wanyakuzi wa mashamba  katika kaunti hiyo hawataruhusiwa kamwe kufanya maendeleo katika mashamba hayo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea hii leo  katika mji wa Kisii, kwenye kongamano lililoandaliwa katika ukumbi wa utamaduni (kisii cultural hall) lililojumuisha wananchi wa kaunti hiyo, Onderi alisema serikali ya kaunti, haitawaruhusu wanyakuzi wa mashamba kufanya maendeleo katika mashamba hayo.

Wakati huo huo,waziri huyo alisema wale ambao wamejenga vibanda vya kufanyia biashara karibu na kanisa la kiadventista la Kisii bila idhini ya serikali hiyo, waondoke mara moja la sivyo waondolewe na serikali.

“Nawaomba kwa unyenyekevu, wale wanabiashara waliojenga vibanda usiku katika eneo liloko karibu na kanisa ya kiadventista bila ruhusa kutoka kwa serikali ya kaunti waondoke kwa hiari kabla hamjaondolewa na serikali,” alisema Onderi.

Haya yanajiri baada ya mwanabiashara Jane Onsongo, kulalamika kuwa alikatazwa kujenga kibanda  katika eneo hilo na amekuwa akifanya biashara katika eneo hilo kwa muda mrefu .

“Nilipowaliza wale  ambao tayari wamejenga, mbona hao wakaruhusiwa kujenga, nami nilikatazwa mmoja wao akasema aliambiwa na afisaa mmoja wa serikali ya kaunti hiyo ingawa hakumtaja afisa huyo jina lake,” alihoji Onsongo mwanabiashara.

Aidha, serikali ya kaunti ya Kisii imesimama kidete kwa kusema kuwa shamba la eneo la Nyambera lililonyakuliwa haitaruhusu mnyakuzi huyo kutumia shamba hilo kamwe.

 Visa vya unyakuzi wa mashamba vimekuwa vikishuhudiwa katika Kaunti hiyo kwa muda mrefu sasa, jambo ambalo lilimlasimu Gavana wa kaunti hiyo James Ongwae, kuomba wananchi wa kaunti hiyo kushirikiana naye kuwafukuza wanyakuzi hao ili maendeleo kuendelea kufanywa na serikali ya kaunti hiyo.

“Mkiona tunapambana na wanyakuzi wa mashamba yenu,nawaomba mshirikiane namimi ili wanyakuzi hao waende na mashamba yawe yakisalia nchini ya uongozi wa kaunti yenu ,” alisema Ongwae.