Mkubwa wa madakatari amesema kuwa wanawake wengi huacha kupeleka watoto wao kliniki pindi wafikiapo miaka miwili.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Johnstone Maneno daktari mkuu katika kituo cha afya cha Ziwa la ng’ombe kilichoko eneo bunge la nyali mjini Mombasa amesema kuwa hali hiyo bado inamuweka mtoto katika hatari ya kupata magonjwa ambayo huenda yakamtatiza kiafya.

Akizungumza katika kituo hicho cha afya akiwa hospitalini hapo kwenye ofisi yake, Maneno alisema kuwa kulingana na hali halisi wamama wanatakikana kutembelea kituo cha afya yani kliniki pindi tu anapotunga mimba na tena kuendelea mpaka pale atakapo zaa na tena kuendelea kumpeleka mtoto mpaka atakapotimu umri wa miaka mitano.

Maneno ameongeza kuwa wamama hao wengi huacha kuwapeleka watoto wao kliniki kwa sababu ambazo hata si za msingi na kupelekea hata wengine kuacha kuenda kliniki pindi tu wanapozaa.

Aidha ametoa onyo kwa akina mama ambao huwa hawawapeleki watoto wao kliniki hadi wanapotimu miaka mitano kuwa wanaweka maisha ya watoto wao katika hatari kubwa sana.

Hata hivyo ametoa hakikisho kuwa ametoa ombi kwa serekali ya kaunti ya Mombasa kuwa kuwe na kampeni ya kutoa hamasisho kwa kina mama kupitia wizara ya afya  ili waweze kupata hii elimu nasaha na pindi tu hilo litakapofanyika mabadiliko yatashuhudiwa.