Kamati ya wafanyikazi katika kaunti ya Kisii imeombwa wanapofanya ajira ya kuajiri wahudumu wa afya katika kaunti kuwapa nafasi za kwanza wale ambao wamekuwa wakijitolea kufanya kazi hiyo bila malipo katika hospitali mbalimbali za kaunti hiyo
Hii ni baada ya kubainika kuwa wahudumu wa afya 1,500 katika kaunti hiyo wamekuwa wakifanya kazi kwa kjitolea kwa muda mrefu bila malipo yeyote.
Spika wa bunge la kaunti ya Kisii Okerosi Ondieki aliomba kamati hiyo kuwaajiri wale ambao walikuwa wamejitolea kupeana huduma za matibabu bila malipo.
Okerosi alisema hayo baada ya Mwakilishi wa wadi ya Magenche kaunti ya Kisii Timothy Ogugu kufikisha ripoti hiyo mbele ya bunge la kaunti jambo ambalo lilijadiliwa na kupitishwa na wengi.
“Naomba Kamati ya wafanyikazi mnapofanya ajira kwa wahudumu wa afya muwape kipaumbele wale ambao wamekuwa wakijitolea kufanya kazi hiyo ya afya bila malipo katika hospital tofauti za kaunti,” alisema Ondieki.