Naibu wa chifu kata ndogo ya Gekonge kata ya Bokeira Hezron Ongaro ameiomba serikali kuu kuwalipa maafisa wa nyumba kumi angalau kitu kidogo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wahandishi wa habari katika kata ya Bokeira, Ongaro alisema kwamba kumekuwa na shida kubwa kwa kuwa hao maafisa wa nyumba kumi hufanya kazi kwa ihiari yao na kama kawaida ni vigumu mtu kufanya kazi kama hiyo ngumu bila kiinua mgongo.

"Hawa maafisa huzunguka nasi kufanya kazi ilihali hawapewi hata sabuni, wala kurunzi, naomba serikali kuu iangalie swala hilo kwa umakini na iweze angalau kuwapea kakitu tu ka kuwatia moyo," alisema naibu wa chifu huyo.

Ongaro aliongeza kwamba imekuwa shida kufanya kazi, na kuwa wengi wa maafisa hao wameiacha kazi hiyo kwa kuwa inawalazimu kuacha kazi zao na kushughulikia wanainchi ilihali hawapati kitu.

"Wao huacha kazi zao za kila siku ili kusuluhisha maswala na wananchi, na warudipo makwao wanalazimika kulala njaa kwa kuwa kazi wameifanya haikuwa na malipo," aliongeza.

Mwandishi alipozungumza na mmoja wamaafisa hao alisema kazi hiyo inamwathiri pakubwa na ni vigumu kutaftutia familia yake chakula cha kila siku.

"Kwangu swala la njaa lilibisha hodi nilipochaguliwa kuwa mwenye kiti wa nyumba kumi sababu kila siku kuna shida ambayo yafaa niitatue ama nirudishe ripoti kwa chifu ama kuna mkutano yafaa nihidhurie, kwa hivyo, kwangu sifanyi majukumu yangu ipasavyo," alisema mmoja wao.