Wapenzi wawili wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuwatusi maafisa wa usalama.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Washtakiwa hao, Ismail Gadaf na Tima AbdulKarim wanadaiwa kuwatusi maafisa wa polisi Bonface Wanjala na Moses Micheal, waliokuwa wakipiga doria katika eneo la Aproved huko Likoni, mnamo Mei 20, 2016.

Wawili hao walikanusha mashtaka hayo siku ya Jumatatu mbele ya Hakimu Francis Kiambi.

Hakimu Kiambi aliagiza wawili hao kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000 ama shilingi 20,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itasikizwa Julai 19, 2016.