Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho amesema kuwa ana imani wakaazi wa kaunti hiyo watamchagua kuhudumu kama gavana kwa hatamu ya pili katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea baada ya kuzuru Hospitali Kuu ya Mkoa wa Pwani siku ya Jumatatu, Gavana Joho alisema kuwa wapinzani wake wanaogombea kiti hicho hawana sera maalum za kufanya maendeleo bali ni tamaa tu.

Joho alisema kuwa hatua zake za maendeleo ndizo zimewakera wengi wao huku akisema kuwa ameibadilisha sekta ya afya katika kaunti hiyo, kwa kutoa vifaa vya kisasa za matibabu, zikiwemo machine ya kuuguza ugonjwa wa saratani.

“Nimeleta mfumo wa kupea wanafunzi maziwa shuleni jambo ambalo halijatekelezwa na serikali ya kaunti yoyote,” alisema Joho.

Joho aliwataja wapinzani wake ambao wamejitokeza katika kinyanganyiro hicho wakiwemo Seneta wa sasa Omar Hassan, Mbunge wa Nyali Hezron Awiti, na mfanyibiashara Suleiman Shahbala kama maadui wa maendeleo ambao hawagependa kuona kaunti hiyo ikiendelea.