Wakaazi wa eneo la Ukanda wa Pwani wamehimizwa wazingatie lishe bora kila wakati.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Mwenyekiti wa Baraza la Madaktari wa Tiba Asilia Nchini Daktari Farsy Ali Abdullahi, alisema kuwa asilimia kubwa ya maradhi ya kuambukiza katika eneo la Pwani husababishwa na ukosefu wa lishe bora.

Daktari Farsy alieleza kuwa asilimia kubwa ya watu hupenda vyakula vya kisasa vilivyo na mafuta mengi yanayochangia maradhi.

Vile vile, mtaalamu huyo wa tiba asilia aliwataka wanawake hususan walio na ujauzito wapunguze kutumia vyakula vya mafuta na wazingatia lishe bora.

“Tunawahimiza wanawake waliyo wajawazito kujiepusha na vyakula vya mafuta ili kuepukana na maradhi ya kuambukiza na wazingatie lishe bora na wakaazi pia wajiepushe na vikala hivyo,” alisema Daktari Farsy.