Mgombea wa kiti cha eneo bunge la Kilifi Kazkazini Pascal Maitha katika hafla ya awali. [Picha: Pascal Maitha/ facebook.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongozi wa Chama cha Kadu Asili wamewataka Wapwani kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kuimarika.Mgombea wa kiti cha eneo bunge la Kilifi Kazkazini Pascal Maitha alisema kuwa hatua ya baadhi ya Wapwani kuunga mkono vyama vingine na kusahau chama hicho chenye asili ya Pwani ni ya kushangaza.“Hiki ndicho chama cha Pwani lakini Wapwani wamekisahau kabisa na wanaunga mkono vyama vingine,” alisema Maitha.Wito wa Maitha unajiri huku baadhi ya wanasiasa waliokuwa wakikiunga mkono chama hicho akiwemo Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga wakikihama na kujiunga na vyama vyengine.Aidha, Maitha alisema kuwa chama hicho kinaendeleza mpango wa kuwasajili wanachama zaidi kutoka maeneo yote ya Kenya.“Tuna imani ya kupata wafuasi wengi zaidi katika chama chetu na tunawakaribisha nyote,” alisema Maitha.