Kundi la wanawake vijana linalojiita 'Wrembo na UhuRuto' katika kaunt ya Mombasa wameanza kutekeleza uhamasisho kwa wanawake ili kujitokeza na kuwania viti vya uongozi kamavile ugavana.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea katika mkutano wao wa kwanza katika uwanja wa makadara siku ya Jumamosi mwenyekiti wa kundi hilo Amina Hussein amesema kuwa wao wanaunga mkono serikali ya Jubilee na wana imani kwa rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto.

Hussein amesema kuwa nia yao si kuwashawishi vijana kujiunga na serikali tu bali pia umuhimu wa vijana kuwa uongozini haswa wanawake na pia kuwasihi vijana kuchukua kura.

Kundi hilo limesema litaendelea na zoezi hilo hadi wakati wa uchaguzi na watakuwa wanawasilisha ombi la kukutana na Rais na Naibu wake ili kuwaeleza matakwa ya vijana.