Idara ya trafiki mkoani Pwani imetoa tahadhari kwa wasafiri wote ambao watakuwa wakisafiri wakati huu wa msimu wa krismasi kuwa waangalifu zaidi ili kuepukana na matapeli wanaokata tiketi za bandia.
Afisa wa dharura katika idara ya trafiki, Njuguna Solomon mkoani Pwani amesema abiria wanaotaka kusafiri wanapaswa kwenda kwa afisi maalumu ambazo zinatambulika na serikali ili kuepuka kutapeliwa.
Hata hivyo Solomon ameelezea kuwa abiria ambao wanatashwishi yoyote kuhusiana kampuni ya kukatia basi wanatakiwa kutoa ripoti haraka katika vituo vya polisi.
Solomon ametoa onyo kwa madereva wote wazembe wanaoendesha magari ya abiria bila kuzingatia sheria za barabarani huku akiwataka madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari ili kuzuia ajali za mara kwa mara za barabarani ambazo zimekuwa zikishuhudiwa.