Tamasha la Mombasa Rocks Music Festival lililozua gumzo na hisia tofauti miongoni mwa Wakenya limeendelea kupewa uzito zaidi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya kutangazwa kuwa msanii maarafu kutoka Marekani Chris Brown na mwenzake Wizkid kutoka Nigeria watakwaa jukwaa moja na wasanii tajika kutoka nchi jirani ya Tanzania.

Mflame wa sauti na kughani katika muziki wa kizazi kipya Ali Kiba na Venessa Mdee wanatarajiwa kuongeza mvuto na kulipamba tamasha hilo zaidi.

Akidhibitisha habari hizo kupitia ukurasa wake wa instagramu, Vanessa aliandika “Mombasaaaa its Me N U this weekend @mombasarockfestival#Juu#Niroge.” 

Tamasha hilo litakalofanyika katika mkahawa wa Nyali Golf Club jijini Mombasa siku ya Jumamosi limeandaliwa na watu binafsi na wala sio serikali ya Kaunti ya Mombasa.

Hata hivyo, serikali ya kaunti imefurahishwa na tamasha hilo ambalo linatarajiwa kupanua jiji la Mombasa kibiashara na pia katika sekta ya utalii.