Washiriki wa kanisa ya Ruthland ya eneo la Ogango iliyoko wilaya ya Nyamira Kaskazini wako na kila sababu ya kutabasamu, baada ya kanisa hilo kubadilishwa kuwa parokia la kwanza katika kaunti ya Nyamira.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kanisa hilo lilibadilishwa kuwa parokia kupitia askofu wa makanisa ya Ruthland nchini Walter Obare, ambaye alisema kanisa hilo sasa litamchagua mmoja wa wahubiri wa kanisa hilo  kuwa kasisi ambaye ataliongoza na kusimamia shughuli zote za kanisa hilo

Askofu Obare, aliwataka washiriki wote wa kanisa hilo kuwa na ushirikiano kati yao ili kuendeleza injili.

Wakiongea na mwandishi huyu siku ya Jumanne katika kanisa hilo la Ogango, washiriki walikiri kuwa wamefulahishwa  na hatua  iliyochukuliwa na askofu Obare kwa kulibadilisha kanisa hilo kuwa parokia, na kusema ni njia mojawapo ya kuwapa motisha na kusambaza injili kila sehemu katika kaunti ya Nyamira.

“Tuko na furaha isiyo na kifani kwa askofu wetu kwa kutuletea Barokia la kwanza katika kaunti ya Nyamira ambalo ni la kanisa yetu,” alihoji mshiriki mmoja wa kanisa hilo.

“Ni rahisi kuwaleta pamoja washiriki wengine kutoka kanisa zetu mbalimbali na kulishwa mkate wa injili tukiwa pamoja ikilinganishwa na hapo mbeleni maana haikuwa rahisi kuwaleta washiriki pamoja,” aliongezea Obino.

Kanisa hilo la Ogango sasa lina kibarua cha kumchagua nani atawawakilisha kama kasisi wa kwanza na kwa siku sijazo, na kusambaza injili kwa watoto wa Mungu.