Vijana 17 waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika na visa vya uhalifu wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Upande wa mashtaka ulielezea Mahakama siku ya Ijumaa kuwa vijana hao walikamatwa siku ya Jumapili, wiki iliyopita, katika maeneo ya Buxton, wakiwa wamejihami kwa panga na visu, wakidaiwa kutaka kutekeleza wizi wa kimabavu.

Jaji Irene Ruguru aliagiza vijana hao wenye umri kati ya 12-26, kuachiliwa kwa dhamana.

Vijana watano wenye chini ya umri wa miaka 18 waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu tano pesa taslimu, huku hao wengine wakiachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 20 pesa tasilimu.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 30 mwezi Mei.