Maafisa wa polisi na wakaazi nje ya duka lililobomolewa. Picha/NMG

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Polisi kutoka eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi hapo jana walifaulu kuwakamata washukiwa sita wanaohusishwa na kisa ambapo mwanamme mmoja alipigwa risasa na kuaga dunia huku mmoja akijeruhiwa katika kisa hicho.

Inasemekana kuwa washukiwa hao wa ujambazi walivunja na kuingia ndani ya duka moja mwishoni mwa juma katika eneo la sosoni katika kaunti ndogo ya Magarini ambapo walitekeleza uhalifu huo

Kulingana na mkuu wa upelelezi eneo hilp Boas Obeto,ni kwamba wahalifu hao waliiba takribani shilingi elfu thelathini kutoka kwa duka hilo jambo ambalo limewafanya wakaazi wa eneo hilo kuishi kwa hofu kwa kuhofia usalama wao

“wakaazi wengi wanaishi na wasiwasi sana kwani wezi waliiba shilingi elfu thelathini na kutekeleza mauaji ambayo mtu mmoja alifariki huku mmoja akijeruhuwa,” Alisema Obeto.

Obeto aliongeza kuwa idara yake imeanzisha uchunguzi kuhusiana na uhalifu huo na kuwahakikishia wakaazi kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.

‘‘Tutahakikisha kuwa kila mtu aliyehusika na mauaji haya amechukuliwa hatua za kisheria.Musihishi kwa hofu,’’ Aliongeza Obeto.

Muathiriwa aliyejeruhiwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Magarini