Vijana wanne wamefikishwa katika mahakama ya Mombasa na kufunguliwa mashtaka ya kuwa wanachama wa kundi la Al-Shabab.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kassim Ali Ahmed, Mohamed Kassim, Ali Mohamed Bwanad na Mustafa Kheri wanadaiwa kuwa na uhusiano na kundi la Al-Shabab.

Aidha, wanne hao wanakabiliwa na madai ya kupatikana na bunduki moja na risasi saba katika eneo la Majengo mnamo Januari mwaka huu.

Siku ya Alhamisi, hakimu mkuu Susan Shitub aliagiza washtakiwa hao kuzuiliwa katika gereza la Shimo La Tewa.

Shitub atatoa uamuzi wa kuwaachilia dhamana kwa washtakiwa hao siku ya Ijumaa.