Vijana saba wanaodaiwa kuwa wa kundi la Wakali Kwanza, wenye chini ya umri wa miaka 18, wameshtakiwa kwa kosa la wizi wa mabavu katika Mahakama ya Mombasa.
Vijana hao wanadaiwa kuwavamia na kuwaibia Grace Neema na Dan Otieno simu zao zenye thamani ya shilingi elfu 20 katika eneo la Tudor, mnamo Agosti 9.
Mmoja wa vijana hao ni mwanafunzi wa Shule ya upili ya Istiqama.
Washukiwa hao walikanusha mashtaka hayo siku ya Jumatano, na kutozwa dhamana ya shilingi elfu 50 ama shilingi elfu 30 pesa taslimu.
Mahakama pia imewataka vijana hao kufanyiwa uchunguzi wa umri kabla mahakama kutoa hukumu yake.
Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 22, mwaka huu.