Vijana watatu wenye umri wa makamo wanaokabiliwa na tuhuma za mauaji watazuiliwa korokoroni kwa muda wa siku 10 ili kutoa nafasi kwa uchunguzi kukamilika.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Watatu hao, Mwasudi Mwazinje, Robbert Waliyaula na Moses Kimani wanadaiwa kumvamia na kumuuwa Janet Odhiambo katika makazi yake huko Kizingo mnamo Juni 7, mwaka huu.

Hii ni baada ya afisa wa uchunguzi Dancan Amoyo kuomba muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wake.

“Naiomba mahakama inipe muda zaidi ili niweze kumaliza uchuguzi wangu wa kesi hii,” alisema Amoyo.

Washukiwa hao walikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Lilian Lewa.

Hakimu Lewa alikubali ombi hilo la kesi hiyo kuendelea baada ya muda wa siku kumi.

Watatu hao walitiwa mbaroni mnamo Julai 8, 9 na 11 mwaka huu.