Washukiwa wawili wa mauaji ya watu 12 mwaka wa 2014, huko Hindi Kibokoni Kaunti ya Lamu, wamepatikana na kesi ya kujibu.
Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi Jaji Martin Muya alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa ni dhahiri kuwa wawili hao, Swaleh Shebe Auni na Joseph Chege Kimani walihusika katika mauaji hayo.
Washukiwa hao wanatarajiriwa kujitetea dhidi ya madai hayo mnamo Februari 11 na 12, 2016 kabla ya kuhukumiwa.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa washukiwa hao wanadaiwa kuhusika katika mauaji ya watu 12 huko Hindi kaunti ya Lamu, kati ya tarehe Julai 5 na 6, 2014.