Mahakama kuu ya Mombasa imewaachilia huru, washukiwa wawili waliokuwa wanakabiliwa na mauaji ya watu 60 eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu mwaka 2014.
Mshukiwa, Diana Salim na Mahadi Swaleh wanadaiwa kuwa kati ya Juni 15, 2014 na 17, 2014, wawili hao walihusika katika mauwaji ya watu 60.
Jaji Muya, aliesema kuwa afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma imekosa kuwasilisha ushahidi wa kutosha dhidi ya washukiwa hao.
Siku ya Jumanne, Muya , alisema kuwa ushahidi wa mashahidi 32 wa kesi hiyo umekosa kuthibitisha kuhusisha wawili hao na mauwaji ya Mpeketoni na Kaisari.
Muya, aliongeza kuwa maafisa wa upelelezi walishindwa kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusiana na waliohusika katika mauwaji hayo.