Vijana wanne wanaokabiliwa na makosa ya ubakaji ywa mtoto wa umri wa miaka 10 na kisha kumuambukiza ukimwi wamenyimwa dhamana katika mahakama ya Mombasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Siku ya Alhamisi, upande wa mashtaka umeiambia mahakama kuwa wanne hao, Issack Musembi, Komu Muthin, Onesmus Mbuvi na Mutingo Kimeo wanadaiwa kutekeleza ubakaji huo kati ya Septemba mwaka jana na Aprili mwaka huu katika eneo la kitongoji duni cha Moroto.

Washtakiwa hao wanadaiwa kumdanganya mtoto huyo kwa pesa na peremende kisha kufanya mapenzi naye.

Wote wamekanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu Diana Mochache.

Kesi hiyo itatajwa Aprili 20, 2016.