Mahakama ya Mombasa imewaachilia wasichana wanne waliokamatwa eneo la Elwak kwa tuhuma za ugaidi kwa dhamana ya shilingi laki tano.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ummulkheir Abdullah, Mariam Said Aboud na Khadija Abubakar walikamatwa eneo la Elwak, huku Halima Aden akikamatwa katika Kaunti ya Machakos kwa tuhuma za ugaidi mwaka wa 2015.

Wasichana hao wamekaa rumande kwa takribani miaka miwili sasa tangu kukamtwa kwao.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Henry Nyakweba alisema ni haki ya kila mshukiwa kikatiba kuachiliwa kwa dhamana..

“Wasichana hawa wamekaa rumande sana huku haki zao zikizidi kukuikwa. Sina budi kuwaachilia kwa dhamana,” alisema Hakimu Nyakweba.

Hii ni mara ya nne kwa wasichana hao kupewa dhamana na baadaye kufutiliwa mbali na mahakama kuu.