Mmiliki wa duka moja katika eneo la Egesieri anaendelea kuuguza majeraha makali ya panga kwenye hospitali kuu ya kaunti ya Nyamira baada ya kushambuliwa na washukiwa wa uhalifu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mokua Guto alijeruhiwa usiku wa kuamkia hii leo, Alhamisi, baada ya wezi hao kumvamia na kuondoka na mali kiasi kisichojulikana.

Kulingana na naibu chifu wa kata ndogo ya Bomanyanya Joseph Kinaro, wahalifu hao walivamia duka hilo majira ya usiku wa manane, ndiposa wakatekeleza uhalifu huo.

Ikumbukwe kwa muda sasa visa vya utovu wa usalama vimekuwa vikiripotiwa katika maeneo mengi kaunti ya Nyamira, hali inayowaacha wengi na maswali iwapo idara ya usalama inatekeleza majukumu yake inavyostahili.