Mshirikishi wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa akiwahutubia wanahabari hapo awali. Amesema kuwa washukiwa zaidi ya wanane wamekamatwa tangu kuanzishwa kwa oparesheni dhidi ya dawa za kulevya nchini. Picha/standardmedia.co.ke
Washukiwa watano wa ulanguzi wa dawa za kulevya waliotiwa mbaroni siku ya Jumatatu watazuiliwa kwa muda wa siku tano ili kutoa nafasi kwa maafisa wa polisi kufanya uchunguzi.
Watano hao, ikiwemo Swaleh Yusuf na mkewe Asma Abdallah Mohamed, walinaswa katika maeneo tofauti jijini Mombasa na katika Kaunti ya Kilifi wakiwa na shilingi milioni 18 na kilo 15 za heroini.Kulingana na mshirikishi wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa, washukiwa zaidi ya wanane wamekamatwa tangu kuanzishwa kwa oparesheni dhidi ya dawa za kulevya nchini.“Tayari tumewatia mbaroni zaidi ya washukiwa wa ulanguzi wanane na tutazidi kuwasaka wengine hadi tutakapo angamiza janga hili,” alisema Marwa.Vita dhidi ya dawa za kulevya vilipamba moto siku chache baada ya wana wa Akasha na raia wawili wa kigeni kusafirishwa hadi nchini Marekani kufunguliwa mashtaka ya ulanguzi wa mihadarati.