Washukiwa watatu wa ulanguzi wa bangi walowasilishwa mbele ya mahakama kuu ya Nakuru wameachiliwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Washukiwa hao Peter Kinyonga ,Peter Ndungu na mwenzao Stephen Chege walishikwa katika maeneo tofauti tofauti katika jimbo la Nakuru wakisafirisha dawa hizo za kulevya.

Wa kwanza Peter kinyonga, alishtakiwa kwa kosa la kuwa na bangi yenye dhamani ya shilingi elfu ishirini ambayo ni kinyume cha sheria.

Mshukiwa wa pili Peter Ndungu naye alipatikana na kosa la kuwa na bangi ya shilingi mia mbili huku wa tatu peter Chege akipatikana na kosa la kuwa na bangi ya shilingi elfu moja.

Wakiongea hii leo mbele ya jaji Doreen Mulekyo watatu hao walikiri kosa lao huku wakikanusha kwamba wao ni walanguzi wa madawa ya kulevya.

Kizungumkuti kilitokea pale ambapo kiongozi wa mashtaka aliulizwa kutoa ushahidi wake kudhibitisha kuwa watatu hao walikuwa wamehusika katika uhalifu.

Alisisitiza Kuwa chemi chemi za dawa hizo za kulevya zilikuwa kwenye mahabara ya Serikali zikifanyiwa uchunguzi.

Ilikuwa ni afueni kwa washtakiwa hao baada ya jaji wa kesi hio kuwaondolea mashtaka kwa kushindwa kwa kiongozi wa mashtaka kuleta idhibati mbele ya korti.

Aliwahimiza maafisa wa polisi kuwa waangalifu zaidi wanapowasilisha kesi mahakamani ili kuzuia hitilafu kama hizo ambazo zilisababisha kuachiliwa huru kwa washtakiwa.

Watatu hao waliondoka mahakamani huku wakionekana wenye furaha na kuahidi kutoyarudia makosa yao.