Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Washukiwa wawili wa ulanguzi wa Pembe za kifaru watajua hatima yao hii leo, Ijumaa iwapo wataachiliwa kwa dhamana ama kusalia rumande.

Hii ni baada ya wakili wao John Magia kuiomba mahakama siku ya Alhamisi kuwaachilia kwa dhamana wateja wake kwa kile alichokitaja kama haki yao kikatiba.

Hatua hii imepingwa na mwendesha mashtaka Erick Masila kwa kusema kuwa bado uchunguzi dhidi yao haujakamilika, na kuitaka mahakama kuwapa muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi dhidi ya washukiwa hao.

Upande wa mashtaka unadai kuwa wawili hao wanatuhumiwa kufadhili kwa ugaidi na ulanguzi wa mihadarati kaunti hii.

Washukiwa hao, Ali Omar Haji na Said Alfani Mwinyi wanadaiwa kupatikana na pembe za kifaru zenye thamani ya shilingi milioni tat mnamo Disemba 27, 2016 katika eneo la Mamangina.