Hakimu Diana Mochache alisema kuwa upande wa mashtaka haujawasilisha sababu za kutosha za kuwazuilia washukiwa hao korokoroni. [Picha/ web.de]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama ya Shanzu imewaachilia jamaa watatu wa familia moja waliokuwa wanazuiliwa kwa madai ya ulanguzi wa watu.Watatu hao wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50 kila mmoja.Zubair Deen, Shama Deen na Zeba Deen walitiwa mbaroni mnamo Disemba 30 eneo la Nyali kwa madai ya kuwaficha wanawake 10 kwenye klabu yao iliyoko eneo la Nyali.Akitoa uamuzi wa kuwaachilia washukiwa hao siku ya Jumanne, Hakimu Diana Mochache alisema kuwa upande wa mashtaka haujawasilisha sababu za kutosha za kuwazuilia washukiwa hao korokoroni.“Sioni sababu kuu za kuwazuilia korokoroni kwa muda Zaidi. Nimeamuru waachiliwe kwa dhamana ya shilingi elfu 50 kila mmoja,” alisema Hakimu Mochache.Haya yanajiri baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kutaka washukiwa hao watatu kuziliwa korokoroni hadi uchunguzi utakapo kamilika.Watatu kati ya wanawake kumi waliokuwa wakifichwa na washukiwa hao ni raia wa India huku saba wakiwa raia wa Nepal.Raia hao watatu wa India waliachiliwa huru baada ya ubalozi wa India kuingilia kati.