Mahakama mmoja ya Mombasa imewaachilia huru vijana watatu kutoka Likoni baada ya kutiwa mbaroni miaka miwili iliyopita.

Share news tips with us here at Hivisasa

Athman, Rashid na mwenzao walionesha furaha baada ya kuondolewa mashtaka ya wizi wa mabavu pamoja na makosa mengine.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, Hakimu Julius Nange'a alisema kuwa maafisa wa usalama walikosa kuwasilisha ushahidi wa kutosha mahakamani.

Watatu hao walikuwa wakikabiliwa na shtaka la kumuibia Neema Juma mnamo tarehe Septemba 10, 2014.

Inadaiwa kuwa vijana hao walitekeleza wizi huo wakiwa wamejihami na silaha ikiwemo panga na nyuta.

Aidha, walikabiliwa na shtaka la kumuibia Mwakini Khamisi, mhudumu wa bodaboda simu ya mkononi pamoja na shilingi elfu 3,600.

Vijana hao walitiwa mbaroni siku tofauti katika eneo la Likoni mnamo Septemba, 2014.