Washukiwa watano wa mauaji watasalia korokoroni kwa siku 14 kusubiri uchunguzi dhidi yao kukamilika.

Share news tips with us here at Hivisasa

Watano hao, Ismail Mutua, Mfaki Nuru, Hassan Abdallah, Tsuma Said na Stephen Musete ambao wanadaiwa kumuua Omar Shafi kwa dhana kuwa alikuwa mwizi mnamo Juni 7, mwaka huu.

Haya yanajiri baada ya afisa mpelelezi Kelvine Wachuri kuomba muda kutoka kwa mahakama kukamilisha uchunguzi dhidi ya washukiwa hao.

“Ningependa kupewa muda wa siku 14 kukamilisha uchunguzi wa mauaji hayo, ili niweze kuwasilisha ushahidi wa kutosha,” alisema Wachuri.

Hakimu Lilian Lewa amekubali ombi hilo la kuwazuia vijana hao kwa siku 14.

Kutokana na madai hayo, huenda marehemu ambae alizikwa muda mfupi baada ya kuuawa akafukuliwa kwa uchunguzi ili kubaini ukweli wa swala hilo.