Wasiwasi unashuhudiwa kwenye shamba tata la Ng’ati baada ya wanachama wa ushirika wa Ng’ati kuzozona kuhusu kipande cha ardhi. Inaarifiwa kuwa baadhi ya wanachama wanateta kuwa wamelaghaiwa na wakubwa wa ushirika huo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

MCA wa eneo hilo Kariuki Mujina alisema baadhi ya vijana walivamia vipande vya ardhi vya viongozi wa Ng’ati na kuharibu mimea kutokana na mzozo huo.

Kariuki anadai wanachama halisi wa Ng’ati walinyanyaswa kwenye shughuli ya kugawa ardhi hiyo iliyonunuliwa kwa pamoja na wanachama.

Mwenyekiti wa ushirika huo alisema kuwa uchochezi wa kisiasa ambao unaendelea kuhusiana na swala hilo.

“Kuna siasa ambazo zinachezwa hapa.Tayari tumewaarifu polisi kuhusiana na uchochezi huo lakini hatua bado haijachukuliwa,” Patrick Karanja, mwenyekiti wa Ng’ati, alisema.