Kundi la wasanii linalofahamika kama Wasojali Band limeshtua wengi katika tasnia ya muziki baada ya kubeba tuzo nyingi zaidi katika Pwani Celebrity Awards zilizoandaliwa siku ya Jumamosi katika mkahawa wa English Point Marina.

Share news tips with us here at Hivisasa

Tuzo hizo ambazo hutolewa kila mwaka, hujumuisha wasanii pamoja na watu mashuhuri kutoka Ukanda wa Pwani, ambapo washindi katika vitengo tofauti hutuzwa baada ya kushinda kura.

Msimu huu umeshuhudia kundi hilo likijizolea jumla ya tuzo tatu katika vitengo vya video bora ya mwaka, kundi bora la mwaka na kibao bora cha ushirikiano mwaka huu.

Wasojali hawakuficha furaha yao na kutoa hisia zao kupitia mtandao wa kijamii.

"Shukrani zetu kwanza kwa Mwenyezi Mungu alietupatia ushindi kwa kazi na bidii yetu katika sanaa ya muziki. Pili, shukrani zetu kwa mashabiki wote waliotupigia kura hadi tukaibuka na ushindi, pamoja na producer wetu Noizer kwa kazi nzuri aliyoifanya, bila kumsahauhau Mzazi Kshort na Producer JacksonLoops.

Kundi hilo liko chini ya uongozi wa Athumani Juma na linajumuisha wasanii wanne; Ibrahim Juma kwa jina la usanii Ability, Juma Mbaruk anayefahamika kama Jaybro, Hamisi Muhammed na Idriss Hamisi al maarufu E-driss.